|
Keep InSight Love All Times
|
 |
|
|
|
|
|
|
| featured member |
 | | LorDcUrrEncY | |
|
|
|
|
.. ..
|
|
Kwa mujibu wa upelelezi uliotolewa na shirika la Scotland Yard nchini humo, kijana mmoja mwenye umri wa miaka 16 anashikiliwa kwa kutuhumiwa kuhusika na mauaji hayo ambapo ilidaiwa marehemu aliandika maoni katika ukurasa wa mtuhumiwa katika tovuti hiyo kuhusu tukio ambalo (mtuhumiwa) huyo hakualikwa katika hafla moja ya sherehe.
Msichana mmoja ambaye hakutaka kutajwa jina lake, alisisitiza chanzo cha mauaji hayo akisema marehemu aliandika maoni ya "kipumbavu" katika ukurasa wa kijana mwenzake.
Inasemekana mtuhumiwa huyo ndiye alikuwa ameanza kuandika jambo fulani katika mtandao huo ambapo Salum alilijibu na hivyo kuanzisha mtafaruku huo ambao ulisababisha kifo cha Salum kwa kuchomwa kisu katika kiwanja kimoja cha mpira wa kikapu ambako alikuwa amekwenda kukutana na vijana wenzake.
Habari zaidi zinasema Salum alikutwa njiani "akiwa hoi" pembezoni mwa Barabara ya Devons karibu na kona ya Barabara ya Purdy.
Shuhuda mmoja miongoni mwa waliomsaidia alisema alimkuta Salum amezungukwa na kundi la vijana wenzake wakijaribu kuzuia asivuje damu kwa wingi kutokana na kuchomwa shingoni au kifuani.
"Nilijaribu kumsemesha kwa kumwinua kichwa chake huku tukisuburi gari la wagonjwa ili aendelee kuwa na nguvu," alisema shuhuda huyo akiongeza kwamba, hata hivyo, kutokana na damu kutoka kwa wingi, Salum alizidi kuishiwa nguvu.
Hata hivyo, baada ya kuwasili kwa gari la wagonjwa na kuanza kumhudumia kwa muda, Salum alifariki hapohapo kando ya barabara.
Source:Global publisherstz |
|
| Added by peacemaker | On December 22, 2009,7:37 am | Comment(3) |
|
-
 |
motto
|
| January 3, 2010,3:44 pm |
-
 |
Catunice face book inamatatizo yake,,,, let pipo not make funny of it,,,, be carefull on what u write,,,, |
| April 21, 2010,10:39 am |
-
 |
peacemaker its better that,all people to shift from fb to kislat.
Here is Safe)))
How do You think?? |
| April 21, 2010,11:30 am |
|
|
|
|
|
|
|
|